Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 61

An-Noor 24:61

النور

لَّيْسَ عَلَى ٱلْأَعْمَىٰ حَرَجٌ وَلَا عَلَى ٱلْأَعْرَجِ حَرَجٌ وَلَا عَلَى ٱلْمَرِيضِ حَرَجٌ وَلَا عَلَىٰٓ أَنفُسِكُمْ أَن تَأْكُلُوا۟ مِنۢ بُيُوتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ ءَابَآئِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أُمَّهَـٰتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ إِخْوَٰنِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَخَوَٰتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَعْمَـٰمِكُمْ أَوْ بُيُوتِ عَمَّـٰتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَخْوَٰلِكُمْ أَوْ بُيُوتِ خَـٰلَـٰتِكُمْ أَوْ مَا مَلَكْتُم مَّفَاتِحَهُۥٓ أَوْ صَدِيقِكُمْ ۚ لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَأْكُلُوا۟ جَمِيعًا أَوْ أَشْتَاتًا ۚ فَإِذَا دَخَلْتُم بُيُوتًا فَسَلِّمُوا۟ عَلَىٰٓ أَنفُسِكُمْ تَحِيَّةً مِّنْ عِندِ ٱللَّهِ مُبَـٰرَكَةً طَيِّبَةً ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمُ ٱلْـَٔايَـٰتِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ

Maana

Si vibaya kwa kipofu, wala si vibaya kwa kiguru, wala si vibaya kwa mgonjwa, wala kwenu nyinyi, mkila katika nyumba zenu, au nyumba za baba zenu, au nyumba za mama zenu, au nyumba za kaka zenu, au nyumba za dada zenu, au nyumba za ami zenu, au nyumba za shangazi zenu, au nyumba za wajomba zenu, au nyumba za dada za mama zenu, au za mliowashikia funguo zao, au rafiki yenu. Si vibaya kwenu mkila pamoja au mbali mbali. Na mkiingia katika nyumba, toleaneni salamu, kuwa ni maamkio yanayotoka kwa Mwenyezi Mungu, yenye baraka na mema. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo kubainishieni Aya zake ili mpate kuelewa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Si vibaya kwa kipofu, wala si vibaya kwa kiguru, wala si vibaya kwa mgonjwa, wala kwenu nyinyi, mkila katika nyumba zenu, au nyumba za baba zenu, au nyumba za mama zenu, au nyumba za kaka zenu, au nyumba za dada zenu, au nyumba za ami zenu, (baba mdogo) au nyumba za shangazi zenu, au nyumba za wajomba zenu, au nyumba za dada wa mama zenu, au za mlio washikia funguo zao, au rafiki yenu. Si vibaya kwenu mkila pamoja au mbali mbali. Na mkiingia katika nyumba, toleaneni salamu, kuwa ni maamkio yanayo toka kwa Mwenyezi Mungu, yenye baraka na mema. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo kubainishieni Aya zake mpate kuelewa. [61]

[61] Wenye udhuru kama vile vipofu, viguru, wagonjwa hawana lawama, bali hata nyinyi wazima hamna lawama kula katika nyumba za watoto wenu, kwani hizo ni nyumba zenu. Wala kula katika nyumba za baba zenu, na mama zenu, na ndugu zenu wanaume na ndugu zenu wanawake, au nyumba za ami zenu, au mashangazi zenu, au wajomba zenu, au mama wadogo, dada wa mama zenu, au nyumba ambazo mmewakilishwa kuzitazama, au nyumba za rafiki zenu mnao changanyika nao, ikiwa hamna yaliyo harimishwa humo. Na hayo ikijuulikana kuwa mwenye nyumba ameruhusu yeye au mkewe. Wala hapana ubaya kula humo pamoja au mbali mbali. Na muingiapo katika nyumba toeni salamu kwa waliomo ambao hao ni baadhi yenu kwa umoja wa Dini na ujamaa. Kwani hao ni kama nyinyi. Na maamkio haya ni maamkio yaliyo wekewa Sharia, yenye baraka na thawabu, na pia ndani yake nyoyo hupoa. Na kwa mfano kama huu Mwenyezi Mungu anazifafanua Aya kwa ajili yenu mpate kuelewa waadhi na hukumu ziliomo ndani yake, na mpate kuzifahamu na mzitende.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hawana dhambi watu wenye nyudhuru miongoni mwa vipofu, vilema na wagonjwa, kuyaacha mambo ya lazima ambayo hawawezi kuyatekeleza, kama kupigana jihadi na mfano wake katika vitu ambavyo vinahitajia kwa kipofu awe anaona, na kilema awe mzima, na mgonjwa awe na afya nzuri. Na nyinyi, enyi Waumini, hamna makosa kula kwenye majumba ambayo ndani yake kuna wake zenu na watoto wenu, na hapa yanaingia majumba ya watoto, au majumba ya baba zenu, au mama zenu, au ndugu zenu. wa kiume, au dada zenu, au ami zenu, au mashangazi zenu, au wajomba zenu, au mama zenu wadogo, au kwenye nyumba ambazo mliwakilishwa kuzisimamia wakati wenyewe hawapo, kwa ruhusa yao, au kwenye nyumba za marafiki. Hakuna makosa yoyote kwenu kula mkiwa pamoja au mbalimbali. Na muingiapo kwenye nyumba zinazokaliwa au zisizokaliwa, amkianeni nyinyi kwa nyinyi kwa maamkizi ya Kiislamu, nayo ni «As- salāmu ‘alaikum wa rahmatullāhi wa barakātuh, au As-salāmu ‘alainā wa ‘alā ‘ibādillāhi-s-sālihīn, iwapo hakuna yoyote. Maamkizi haya Allah Mtukufu Ameyaweka, nayo yana baraka, yanakuza kusafishana nia na kupendana, ni mazuri yanayopendeza kwa mwenye kuyasikia. Na kwa mfano wa ufafanuzi huu anawafafanulia Allah Mtukufu alama za Dini Yake na aya Zake, ili mzifahamu na mzitumie.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net