Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 60

An-Noor 24:60

النور

وَٱلْقَوَٰعِدُ مِنَ ٱلنِّسَآءِ ٱلَّـٰتِى لَا يَرْجُونَ نِكَاحًا فَلَيْسَ عَلَيْهِنَّ جُنَاحٌ أَن يَضَعْنَ ثِيَابَهُنَّ غَيْرَ مُتَبَرِّجَـٰتٍۭ بِزِينَةٍ ۖ وَأَن يَسْتَعْفِفْنَ خَيْرٌ لَّهُنَّ ۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Maana

Na wanawake wazee wasiotaraji kuolewa, si vibaya kwao kupunguza nguo zao, bila ya kujishaua kwa mapambo. Na wakijiheshimu ni bora kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanawake wazee wasio taraji kuolewa, si vibaya kwao kupunguza nguo zao, bila ya kujishaua kwa mapambo. Na wakijihishimu ni bora kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. [60]

[60] Na wanawake wakongwe ambao hawatumai kuolewa, hawalaumiwi wakipunguza baadhi ya nguo zao, kwa sharti wasiwe wanajishauwa kwa kuonyesha uzuri wa mwili wao ambao Mwenyezi Mungu ameamrisha usitiriwe. Lakini kujihishimu kwa kujisitiri kwa ukamilifu ni bora kwao kuliko kujifunua. Na Mwenyezi Mungu anawasikia wayasemayo, na anayajua makusudio yao, na atawalipa kwa hayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wanawake wakongwe ambao wamejikalia hawajistareheshi na hawana matamanio kwa sababu ya uzee wao, hawana hamu ya kuolewa na wanaume wala wanaume hawana hamu nao. Wanawake hawa hawana makosa kujitanda sehemu ya nguo zao kama vile shuka, bila kuonesha pambo wala kujirembesha. Na kuvaa kwao nguo hizi, kwa kujisitiri na kujihifadhi, ni uzuri kwao. Na Allah Mtukufu ni Msikizi wa maneno yenu, ni Mjuzi wa nia zenu na matendo yenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net