Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 59

An-Noor 24:59

النور

وَإِذَا بَلَغَ ٱلْأَطْفَـٰلُ مِنكُمُ ٱلْحُلُمَ فَلْيَسْتَـْٔذِنُوا۟ كَمَا ٱسْتَـْٔذَنَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمْ ءَايَـٰتِهِۦ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Maana

Na watoto wanapofikilia umri wa kubaleghe basi na watake ruhusa, kama walivyotaka ruhusa wa kabla yao. Hivyo ndivyo anavyowabainishia Mwenyezi Mungu Aya zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na watoto wanapo fikilia umri wa kubaalighi basi nawatake ruhusa, kama walivyo taka ruhusa wa kabla yao. Hivyo ndivyo anavyo kubainishieni Mwenyezi Mungu Aya zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima. [59]

[59] Na vijana vyenu wakifikilia umri wa kubalighi inawapasa watake ruhusa ya kuingia kila nyumba, na kila wakati, kama ilivyo wapasa wenzao wa kabla yao. Na kwa mfano wa uwazi kama huu Mwenyezi Mungu anakuwekeeni wazi Aya zake alizo ziteremsha. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni Mkunjufu wa ujuzi, Mkubwa wa hikima. Anajua linalo wasilihi waja wake, na anawaatungia Sharia zinazo wanasibu, na kwa kadri ya haja yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na pindi watoto wanapofikia miaka ya kubaleghe na kukalifishwa hukumu za kisheria, ni juu yao watake ruhusa wakitaka kuingia nyakati zote kama wanavyotaka ruhusa watu wazima. Na kama Allah Mtukufu Anavyowafafanulia adabu za kutaka ruhusa (kuingia majumbani), vilevile Anawafafanulia Allah Mtukufu, Aliyetukuka, aya Zake. Na Allah Mtukufu Anayajua sana yanayowafaa waja Wake, ni Mwingi wa hekima katika sheria Zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net