An-Noor 24:58
النوريَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لِيَسْتَـْٔذِنكُمُ ٱلَّذِينَ مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُكُمْ وَٱلَّذِينَ لَمْ يَبْلُغُوا۟ ٱلْحُلُمَ مِنكُمْ ثَلَـٰثَ مَرَّٰتٍ ۚ مِّن قَبْلِ صَلَوٰةِ ٱلْفَجْرِ وَحِينَ تَضَعُونَ ثِيَابَكُم مِّنَ ٱلظَّهِيرَةِ وَمِنۢ بَعْدِ صَلَوٰةِ ٱلْعِشَآءِ ۚ ثَلَـٰثُ عَوْرَٰتٍ لَّكُمْ ۚ لَيْسَ عَلَيْكُمْ وَلَا عَلَيْهِمْ جُنَاحٌۢ بَعْدَهُنَّ ۚ طَوَّٰفُونَ عَلَيْكُم بَعْضُكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمُ ٱلْـَٔايَـٰتِ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ
Enyi mlioamini, na wakukitakeni idhini wale iliyowamiliki mikono yenu ya kulia na walio bado kubaleghe miongoni mwenu mara tatu - kabla ya Swala ya Alfajiri, na wakati mnapovua nguo zenu adhuhuri, na baada ya Sala ya Isha. Hizi ni nyakati tatu za faragha kwenu. Si vibaya kwenu wala kwao baada ya nyakati hizi, kuzungukiana nyinyi kwa nyinyi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowaelezeni Aya zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Nawakutakeni idhini iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia na walio bado kubaalighi miongoni mwenu mara tatu - kabla ya Sala ya alfajiri, na wakati mnapo vua nguo zenu adhuhuri, na baada ya Sala ya isha. Hizi ni nyakati tatu za faragha kwenu. Si vibaya kwenu wala kwao baada ya nyakati hizi, kuzungukiana nyinyi kwa nyinyi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo kuelezeni Aya zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima. [58]
[58] Enyi mlio amini! Yakupaseni muamrishe watumishi wenu na vijana wenu ambao bado hawajabalighi wasikuingilieni vyumbani mwenu ila baada ya kutaka idhini katika nyakati tatu, nazo ni kabla ya Swala ya alfajiri, na pale mnapo punguza nguo zenu wakati wa kupumzika mchana, na baada ya Swala ya Isha mnapo jitayarisha kulala. Kwani nyakati hizi mtu hubadilisha mavazi ya kulalia badala ya mavazi ya kutokea, na huonekana sehemu za mwili ambazo hazifai kuonekana. Wala hapana ubaya kwenu wala kwao kuingia bila ya ruhusa nyakati nyenginezo, kwa sababu ni jamba la ada watu wa nyumbani kupitiana kwa maslaha yao. Na kwa uwazi wa namna hii Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya za Qur'ani ili akuwekeeni wazi hukumu. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni Mkunjufu wa ujuzi, Mkubwa wa hikima, anajua yanayo silihi kwa waja wake, na anawatungia Sharia zinazo wanasibu, na kwa kadri ya haja yao. "Enyi mlio amini! Nawakutakeni idhini iliyo wamikiliki mikono yenu ya kulia na walio bado kubaalighi miongoni mwenu mara tatu - kabla ya Swala ya alfajiri, na wakati mnapo vua nguo zenu adhuhuri, na baada ya Swala ya isha. Hizi ni nyakati tatu za faragha kwenu. Si vibaya kwenu wala kwao baada ya nyakati hizi, kuzungukiana nyinyi kwa nyinyi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo kuelezeni Aya zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima." Aya hii tukufu ni moja katika Aya zinazo elekeza nadhari ya watu wazingatie yaliyo laiki katika jamii za watu khasa ndani ya ukoo. Nayo kuwa kuchanganyika kwa watumishi na watoto katika aila yao huenda kukapindukia mipaka ya hishima za maingiano, wakawa wanawaingilia wenginewe bila ya kutaka idhini katika nyakati maalumu zilizo tajwa katika Aya. Na kwa kuwa nyakati hizo ni nyakati za faragha na uhuru wa binafsi, na kuvua nguo nzito nzito, Aya hii imekusudia kuweka Sharia ya kutaka idhini katika nyakati hizo kutokana na watumishi na vijana ili wasione ambayo yanahisabiwa kuwa ni siri, ambayo ni kama utupu ambao wapasa kusitiriwa. Na kwa hivyo wanaelekezwa watu wa ukoo wavae mavazi yanayo kuwa laiki ya kukabiliana hata wao kwa wao, ili hishima yao ibaki imehifadhika, na uhuru wao umedhaminika, na adabu zao zimechungika. Na Qur'ani ndio inaayo faa khasa kutuongoza tufuate mwendo ulio bora na wa juu. (Ikiwa watoto wa nyumbani haiwafalii kuwaingilia watu katika nyakati hizo za faragha zilizo tajwa, seuze watu mbali!)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi ambao mmemuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifanyia kazi sheria Zake! Waamrisheni watumwa wenu, wajakazi wenu na watoto waungwana ambao umri wao haujafikia wa kubaleghe waombe ruhusa wakitaka kuingia kwenu katika nyakati za mapumziko yenu na kuvua nguo zenu: kabla ya Swala ya Alfajiri, kwa kuwa huo ni wakati wa kuvua nguo za kulalia na kuvaa nguo za baada ya kuamka, na wakati wa kuvua nguo kwa mapumziko ya kipindi cha mchana wakati wa jua kali, na baada ya Swala ya Isha, kwa kuwa huo ni wakati wa kulala. Nyakati tatu hizi ni za kujifunua na kujiacha wazi na kunapungua kujisitiri. Lakini katika nyakati zisizokuwa hizo, si makosa wakiingia bila ya idhini, kwa kuwa wao wanahitaji kuingia kwenu, wao ni wa kuingia na kutoka mara kwa mara kwa kutumwa, na kwa kuwa dasturi iliyozoeleka ni kuwa nyinyi mnatembeleana nyakati hizi kwa kutimiza haja zenu zenye maslahi kwenu. Na kama Alivyowafafanulia Allah Mtukufu hukumu za kutaka ruhusa (ya kuingia majumbani), Anawafafanulia aya Zake, hukumu Zake, hoja Zake na Sheria za Dini Yake. Na Allah Mtukufu Anayajua sana yanayowafaa viumbe Wake, ni Mwingi wa hekima katika upelekeshaji Wake mambo yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net