An-Noor 24:57
النورلَا تَحْسَبَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مُعْجِزِينَ فِى ٱلْأَرْضِ ۚ وَمَأْوَىٰهُمُ ٱلنَّارُ ۖ وَلَبِئْسَ ٱلْمَصِيرُ
Msiwadhanie waliokufuru kwamba watashinda katika nchi. Na makaazi yao ni Motoni, na hakika ni maovu kweli marejeo yao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Msiwadhanie walio kufuru kwamba watashinda katika nchi. Na makaazi yao ni Motoni, na hakika ni maovu kweli marejeo yao. [57]
[57] Ewe Nabii! Usidhani kuwa makafiri wataweza kumkwepa Mwenyezi Mungu asiwashike kwa madhambi yao, au watu wa Haki wasiwaone pahala popote pale katika ardhi. Bali Yeye ni Muweza, na marejeo yao Siku ya Kiyama ni Motoni. Na marejeo maovu kabisa ni marejeo yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Msidhani tena msidhani kwamba wale waliokufuru wanamshinda Allah Mtukufu katika ardhi, kwani Yeye ni Muweza wa kuwaangamiza, na marejeo yao, huko Akhera ni Motoni. Na ni mabaya sana marejeo haya na mwisho huu. Maneno haya ni maelekezo kwa ummah wote, ingawa anayeambiwa hapa ni Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie).
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net