An-Noor 24:56
النوروَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُوا۟ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَطِيعُوا۟ ٱلرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ
Na shikeni Swala, na toeni Zaka, na mtiini Mtume, ili mpate kurehemewa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na shikeni Swala, na toeni Zaka, na mt'iini Mtume, ili mpate kurehemewa. [56]
[56] Na shikeni Swala kwa ukamilifu wa nguzo katika utulivu na unyenyekevu, ili ipate kuwa inazuia uchafu na mambo mabaya. Na wapeni Zaka wanao stahiki. Na mt'iini Mtume kwa yote anayo kuamrisheni, ili mpate kutaraji rehema ya Mwenyezi Mungu na radhi yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na isimamisheni Swala kwa kuitimiza, na toeni Zaka kuwapa wanaostahiki kupewa na mumtii Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kwa kutarajia Allah Mtukufu Awarehemu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net