Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 55

An-Noor 24:55

النور

وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنكُمْ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ كَمَا ٱسْتَخْلَفَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ ٱلَّذِى ٱرْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّنۢ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِى لَا يُشْرِكُونَ بِى شَيْـًٔا ۚ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْفَـٰسِقُونَ

Maana

Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watakaokufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu. [55]

[55] Mwenyezi Mungu amewahidi katika nyinyi, walio sadiki haki na wakaifuata, na wakatenda vitendo vyema, kwa ahadi ya kutia mkazo. Yakwamba atawafanya makhalifa, (wafuatizi) warithi wa wale walio tangulia wawarithi katika kuhukumu na utawala katika nchi, kama ilivyo kuwa hali kwa walio tangulia. na atawasimamishia Uislamu kuwa ndio Dini yako, alio wapendekezea, basi watakuwa na heba na madaraka. Na atabadilisha hali yao ya khofu iwe ya amani, wawe wananiabudu mimi, nao wametua hawanishirikishi mimi na chochote kile katika ibada. Na wenye kukhiyari ukafiri baada ya ahadi hii ya kweli au wakaritadi wakaacha Uislamu, basi hao ndio waliotoka nje walioasi wapizani

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Amewaahidi walioamini miongoni mwenu na wakafanya matendo mema kwamba atawarithisha ardhi ya washirikina na atawafanya ni wasimamizi wa hiyo ardhi, kama alivyofanya kwa waliokuja kabla yao kati ya wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mitume Wake, na Aifanye Dini yao ambayo Ameridhika nayo na Akawachagulia, nayo ni Uislamu, ni Dini yenye ushindi na uthabiti, na Azigeuze hali zao kwa kuwaondolea hofu na kuwaletea amani, iwapo watamuabudu Allah Mtukufu, Peke Yake, na watasimama imara kwa kumtii, na wasimshirikishe na kitu chochote. Na Mwenye kukanusha baada ya hilo la kupewa usimamizi, amani, uthabiti na utawala kamili, na akakanusha neema za Allah Mtukufu, basi hao ndio waliotoka nje ya utiifu kwa Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net