An-Noor 24:54
النورقُلْ أَطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُوا۟ ٱلرَّسُولَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَإِنَّمَا عَلَيْهِ مَا حُمِّلَ وَعَلَيْكُم مَّا حُمِّلْتُمْ ۖ وَإِن تُطِيعُوهُ تَهْتَدُوا۟ ۚ وَمَا عَلَى ٱلرَّسُولِ إِلَّا ٱلْبَلَـٰغُ ٱلْمُبِينُ
Sema: Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume. Na mkigeuka, basi yaliyo juu yake ni yale aliyobebeshwa, na yaliyo juu yenu ni yale mliyobebeshwa nyinyi. Na mkimtii yeye, mtaongoka. Na hapana juu ya Mtume ila kufikisha Ujumbe wazi wazi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume. Na mkigeuka, basi yaliyo juu yake ni aliyo bebeshwa, na yaliyo juu yenu ni mliyo bebshwa nyinyi. Na mkimt'ii yeye mtaongoka. Na hapana juu ya Mtume ila kufikisha Ujumbe wazi wazi. [54]
[54] Waambie: Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume kwa ut'iifu wa kweli wenye kuonyesha vitendo vyenu. Wanaafiki wakipuuza wasifuate, basi juu ya Muhammad ni waajibu wa aliyo twishwa tu na Mwenyezi Mungu, nayo ni amri ya kufikilisha Ujumbe, wala hakukalifishwa uwongofu wao. Na nyinyi juu yenu ni hayo aliyo kutwikeni Mwenyezi Mungu nayo ni kufuata na kut'ii. Na mtapata adhabu ikiwa mtaendelea na uasi. Na mkimt'ii Mtume mtaongoka kwenye kheri. Na yeye haimpasi ila kufikisha kwa uwazi mukimti au mukiamsi na yeye akaisha fikisha
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na useme, ewe Mtume, kuwaambia watu, «Mtiini Allah Mtukufu na mtiini Mtume.» Na wakipa mgongo, basi jukumu la Mtume ni kufanya aliyoamrishwa ya kuufikisha ujumbe, na ni jukumu la watu wote kuyafanya waliyoamrishwa ya kufuata. Na mkimtii yeye mtaongoka. Na jukumu la Mtume ni kuufikisha ujumbe wa Mola wake mafikisho yaliyo wazi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net