An-Noor 24:53
النوروَأَقْسَمُوا۟ بِٱللَّهِ جَهْدَ أَيْمَـٰنِهِمْ لَئِنْ أَمَرْتَهُمْ لَيَخْرُجُنَّ ۖ قُل لَّا تُقْسِمُوا۟ ۖ طَاعَةٌ مَّعْرُوفَةٌ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرٌۢ بِمَا تَعْمَلُونَ
Na wanaapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa kiapo chao ya kwamba ukiwaamrisha kwa yakini watatoka. Sema: Msiape! Utiifu unajulikana. Hakika Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanaapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa kiapo chao ya kwamba ukiwaamrisha kwa yakini watatoka. Sema: Msiape! Ut'iifu unajuulikana. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda. [53]
[53] Na wanaafiki wanaapa kwa ukomo wa nguvu za viapo vyao, kwamba wewe, Muhammad, ukiwaamrisha watoke nawe kwenda vitani watakut'ii. Waambie: Msiape! Kwani mambo yatakikanayo kwenu mnayajua, hapana hata mmoja wenu asiye yajua. Wala yamini zenu za uwongo haziondoi ujuzi huo. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua baraabara kila linalo tokana nanyi, na Yeye atakulipeni kwayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wanafiki waliapa kwa Allah Mtukufu Aliyetukuka, kwa upeo wa juhudi yao, viapo vizito, «Ukituamrisha, ewe Mtume, kutoka kwenda kwenye jihadi pamoja na wewe, tutatoka tena tutatoka» Sema uwaambie, «Msiape viapo vya urongo, kwani utiifu wenu unajulikana kuwa ni wa ulimini tu. Kwa kweli Allah Mtukufu Anayatambua mnayoyafanya, na Atawapa malipo yake».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net