An-Noor 24:52
النوروَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَخْشَ ٱللَّهَ وَيَتَّقْهِ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْفَآئِزُونَ
Na wenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakamwogopa Mwenyezi Mungu na wakamcha, basi hao ndio wenye kufuzu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakamwogopa Mwenyezi Mungu na wakamcha, basi hao ndio wenye kufuzu. [52]
[52] Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na kuridhia anayo yaamrisha Mtume s.a.w. na wakaiogopa dhati ya Mwenyezi Mungu Tukufu, na wakaukumbuka Utukufu wake, na wakaikhofu ghadhabu yake, hao ndio watakao pata radhi ya Mwenyezi Mungu na mapenzi yake, na neema za Pepo, na ndio wenye kupata kheri tupu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mwenye kumtii Allah Mtukufu na Mtume Wake katika kufuata maamrisho, na kujiepusha na makatazo, na akaogopa mwisho mbaya wa uasi, na akajihadhari na adhabu ya Allah Mtukufu, basi hao ndio wenye kufuzu kupata neema Peponi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net