Al-Furqaan 25:1
الفرقانتَبَارَكَ ٱلَّذِى نَزَّلَ ٱلْفُرْقَانَ عَلَىٰ عَبْدِهِۦ لِيَكُونَ لِلْعَـٰلَمِينَ نَذِيرًا
Ametukuka aliyeteremsha Furqani kwa mja wake, ili awe mwonyaji kwa walimwengu wote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ametukuka aliye teremsha Furqani kwa mja wake, ili awe mwonyaji kwa walimwengu wote. [1]
[1] Mambo ya Mwenyezi Mungu yametukuka, na kheri yake imezidi. Yeye ndiye aliye iteremsha Furqani, yaani Qur'ani, ya kufarikisha baina ya kweli na uwongo juu ya mja wake, Muhammad s.a.w., ili awe mwonyaji na mwenye kuifikisha hiyo Qur'ani kwa walimwengu wote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni kubwa mno baraka za Allah Mtukufu na ni mengi sana mema Yake na ni kamilifu sifa Zake, Aliyetakasika na kutukuka, Ambaye Ameiteremsha Qur’ani, yenye kupambanua baina ya ukweli na batili, kwa mja Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), ili awe ni mjumbe kwa binadamu na majini, na awe muonyaji wa adhabu ya Allah Mtukufu kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net