An-Noor 24:38
النورلِيَجْزِيَهُمُ ٱللَّهُ أَحْسَنَ مَا عَمِلُوا۟ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِۦ ۗ وَٱللَّهُ يَرْزُقُ مَن يَشَآءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ
Ili Mwenyezi Mungu awalipe bora ya waliyoyatenda, na awazidishie katika fadhila zake. Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ili Mwenyezi Mungu awalipe bora ya waliyo yatenda, na awazidishie katika fadhila zake. Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu. [38]
[38] Na malipo ya vitendo vyao ni kulipwa sawa sawa kwa ubora wa malipo kwa vitendo vyao vyema, na watapata fadhila kwa kupewa zaidi kuliko wanavyo stahiki. Kwani Yeye Subhanahu ni Mkunjufu wa fadhila, humpa amtakaye katika waja wake wema kipao kikubwa, asichoweza mtu kukihisabu wala wenye kuhisabu hawawezi kukisia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ili Allah Mtukufu Awape malipo mema ya matendo yao mazuri zaidi na Awaongezee kutokana na wema Wake. Na Allah Mtukufu Anamruzuku Anayemtaka bila kumhesabia, bali Anampa malipo ambayo matendo yake mema hayakuyafikia, na pasi na hesabu wala kipimo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net