An-Noor 24:39
النوروَٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ أَعْمَـٰلُهُمْ كَسَرَابٍۭ بِقِيعَةٍ يَحْسَبُهُ ٱلظَّمْـَٔانُ مَآءً حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَهُۥ لَمْ يَجِدْهُ شَيْـًٔا وَوَجَدَ ٱللَّهَ عِندَهُۥ فَوَفَّىٰهُ حِسَابَهُۥ ۗ وَٱللَّهُ سَرِيعُ ٱلْحِسَابِ
Na waliokufuru vitendo vyao ni kama sarabi (mazigazi) uwandani. Mwenye kiu huyadhania ni maji. Hata akiyaendea hapati chochote. Na atamkuta Mwenyezi Mungu hapo naye amlipe hisabu yake sawa sawa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walio kufuru vitendo vyao ni kama sarabi (mazigazi) uwandani. Mwenye kiu huyadhania ni maji. Hata akiyaendea hapati chochote. Na atamkuta Mwenyezi Mungu hapo naye amlipe hisabu yake sawa sawa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu. [39]
[39] Na hao walio pinga na wakakanya wanadhani wenyewe kuwa wamefanya vizuri, na kwamba vitendo vyao vizuri vitawaletea faida Siku ya Kiyama. Lakini hao wamekosea katika dhana yao hiyo. Kwani mfano wa vitendo vyao katika upotovu wake na kukosa maana ni kama mmetuko unao tokea unapo angukia mwako wa jua wakati wa adhuhuri juu ya ardhi tambarare jangwani. Mwenye kiu hudhania kuwa ni maji. Hata akiyafikia asikute chochote chenye manufaa kama alivyo dhania. Hali kadhaalika vitendo vya makafiri siku ya malipo vitakuwa vumbi lilio tawanyika. Na kafiri ataikuta adhabu ya Mwenyezi Mungu inamngojea kwa utimilivu wake bila ya nuksani. Hakika hisabu ya Mwenyezi Mungu hapana shaka inakuja. Na Yeye, Aliye takasika, ni Mwepesi katika kuhisabu kwake, hachelewi wala hakosei.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale waliomkanusha Mola wao na wakawafanya warongo Mitume Wake, matendo yao waliyoyategemea kuwa yatawafaa huko Akhera, kama kuunga udugu, kuwaacha huru mateka na yasiyokuwa hayo, yatakuwa ni kama mangati, nayo ni yale yanayoonekana kama maji juu ya ardhi tambarare kipindi cha mchana cha jua kali, mwenye kiu akiyaona anadhani ni maji, na akiyajia hakuti kuwa ni maji. Basi kafiri anadhani kwamba matendo yake yatamfaa, na ifikapo Siku ya Kiyama atakuta kuwa hayana malipo mema, na hapo atamkuta Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, Anamngojea Ampe malipo ya matendo yake kikamilifu. Na Allah Mtukufu ni mwepesi wa kuhesabu. Basi wajinga wasione kwamba ahadi ya Allah Mtukufu imekawia kuwa, kwani hiyo hapana budi kuja kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net