An-Noor 24:37
النوررِجَالٌ لَّا تُلْهِيهِمْ تِجَـٰرَةٌ وَلَا بَيْعٌ عَن ذِكْرِ ٱللَّهِ وَإِقَامِ ٱلصَّلَوٰةِ وَإِيتَآءِ ٱلزَّكَوٰةِ ۙ يَخَافُونَ يَوْمًا تَتَقَلَّبُ فِيهِ ٱلْقُلُوبُ وَٱلْأَبْصَـٰرُ
Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kushika Sala, na kutoa Zaka. Wanaihofu Siku ambayo nyoyo na macho yatageuka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kushika Sala, na kutoa Zaka. Wanaikhofu Siku ambayo nyoyo na macho yatageuka. [37]
[37] Dunia na yaliomo duniani ya kuuza na kununua hayawashughulishi wakaacha kumdhukuru Mwenyezi Mungu na kumzingatia. Wao wanashika Swala, na wanatoa Zaka, na huku wakiikhofu Siku ya Kiyama ambapo nyoyo zitakuwa hazina utulivu kwa sababu ya wasiwasi na hamu, na kungojea matokeo, na macho yatadahadari kwa mhangaiko na kushtuka kwa vituko vigeni wanavyo viona, na wingi wa vitisho.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanaume ambao hawapumbazwi na ununuzi wala uuzaji na jambo la kumtaja Allah Mtukufu, kusimamisha Swala na kutoa Zaka kwa anayestahiki kupewa; wanaiogopa Siku ya Kiyama ambayo nyoyo zinageukageuka baina ya matumaini ya kuokoka na hofu ya kuangamia, na macho yatakuwa yanageukageuka yanatazama ni mwisho gani yataishia?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net