An-Noor 24:36
النورفِى بُيُوتٍ أَذِنَ ٱللَّهُ أَن تُرْفَعَ وَيُذْكَرَ فِيهَا ٱسْمُهُۥ يُسَبِّحُ لَهُۥ فِيهَا بِٱلْغُدُوِّ وَٱلْـَٔاصَالِ
Katika Nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe, na humo litajwe jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Katika Nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe, na humo litajwe jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni [36]
[36] Hakika wapo watu wanao mtakasa Mwenyezi Mungu na wanamuabudu misikitini ambayo Mwenyezi Mungu ameamrisha ijengwe na iamirishwe kwa kudhukuriwa Mwenyezi Mungu, nao wameshughulikia hayo asubuhi na jioni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Nuru hii inang’ara kwenye misikikiti ambayo Allah Mtukufu Ameamrisha itukuzwe, ijengwe na jina Lake litajwe humo kwa kusoma Kitabu Chake na kuleta tasbihi (subhān Allāh) na kuleta tahlili (Allāh Akbar) na yasiyokuwa hayo katika aina mbalimbali za kumtaja. Wanaswali kwenye misikiti hiyo kwa ajili ya Allah Mtukufu asubuhi na jioni.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net