Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 26

An-Noor 24:26

النور

ٱلْخَبِيثَـٰتُ لِلْخَبِيثِينَ وَٱلْخَبِيثُونَ لِلْخَبِيثَـٰتِ ۖ وَٱلطَّيِّبَـٰتُ لِلطَّيِّبِينَ وَٱلطَّيِّبُونَ لِلطَّيِّبَـٰتِ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ مُبَرَّءُونَ مِمَّا يَقُولُونَ ۖ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ

Maana

Wanawake waovu ni wa wanaume waovu, na wanaume waovu ni wa wanawake waovu. Na wanawake wema ni wa wanaume wema, na wanaume wema ni wa wanawake wema. Hao wameepushwa na hayo wanayoyasema; wao watapata msamaha na riziki ya ukarimu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wanawake waovu ni wa wanaume waovu, na wanaume waovu ni wa wanawake waovu. Na wanawake wema ni wa wanaume wema, na wanaume wema ni wa wanawake wema. Hao wameepushwa na hayo wanayo yasema; wao watapata msamaha na riziki ya ukarimu. [26]

[26] Wanawake waovu ni wa wanaume waovu, na wanaume waovu ni wa wanawake waovu. Na kadhaalika wanawake wema ni wa wanaume wema, na wanaume wema ni wa wanawake wema. Basi yamkini vipi kuwepo uwovu katika wema ulio hifadhiwa nao ni mke wa mwema muaminifu Mtume Mtukufu s.a.w.? Na wema hawa wamehifadhika na tuhuma wanazo wasingizia hao waovu. Na wao wana maghfira ya Mwenyezi Mungu kwa vijidhambi vidogo vidogo ambavyo mwanaadamu hakosekani kuwa navyo. Na watapata ukarimu mkubwa wa kupata neema za Peponi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kila kiovu miongoni mwa wanaume na wanawake, na maneno na vitendo, kinalingana na kiovu na kinaoana nacho. Na kila kizuri miongoni mwa wanaume na wanawake, maneno na vitendo, kinalingana na kizuri na kinaoana nacho. Na wanaume wazuri na wanawake wazuri ni wenye kutakaswa na uovu wanaowasingizia nao wale waovu. Watapata kutoka kwa Allah Mtukufu msamaha utakayoyafunika madhambi yote na riziki njema Peponi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net