Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 27

An-Noor 24:27

النور

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَدْخُلُوا۟ بُيُوتًا غَيْرَ بُيُوتِكُمْ حَتَّىٰ تَسْتَأْنِسُوا۟ وَتُسَلِّمُوا۟ عَلَىٰٓ أَهْلِهَا ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ

Maana

Enyi mlioamini! Msiingie nyumba zisizo nyumba zenu mpaka mwombe ruhusa, na mwatolee salamu wenyewe. Hayo ni bora kwenu ili mpate kukumbuka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Msiingie nyumba zisio nyumba zenu mpaka mwombe ruhusa, na mwatolee salamu wenyewe. Hayo ni bora kwenu mpate kukumbuka. [27]

[27] Enyi mlio amini! Msiingie katika nyumba zisio kuwa zenu ila baada ya kutaka idhini kwa wakaazi wake na mkaruhusiwa kuingia, na baada ya kuwatolea salamu wakaazi wake - na salamu ni bora kwenu kuliko kuingia tu bila ya kutoa salamu. Na Mwenyezi Mungu amekuwekeeni sharia hii ili mpate kunasihika na muifuate.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazitumia sheria Zake, msiingie kwenye nyumba zisizokuwa zenu, mpaka muwatake ruhusa wenyewe ya kuingia na muwaamkie. Na matamshi ya maamkizi hayo yatokayo kwenye Sunnah ni, «Assalāmu ‘alaikum. Je, niingie?» Kutaka ruhusa huko ni bora kwenu nyinyi. Huenda mkazikumbuka, kwa kufanya kwenu hivyo, amri za Allah Mtukufu na mkapata kumtii.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net