An-Noor 24:25
النوريَوْمَئِذٍ يُوَفِّيهِمُ ٱللَّهُ دِينَهُمُ ٱلْحَقَّ وَيَعْلَمُونَ أَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْحَقُّ ٱلْمُبِينُ
Siku hiyo Mwenyezi Mungu atawapa sawa sawa malipo yao ya haki, na watajua kwamba hakika Mwenyezi Mungu ndiye Haki iliyo wazi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Siku hiyo Mwenyezi Mungu atawapa sawa sawa malipo yao ya haki, na watajua kwamba hakika Mwenyezi Mungu ndiye Haki Iliyo Wazi. [25]
[25] Siku hiyo Mwenyezi Mungu atawaadhibu adhabu iliyo kwisha hukumiwa wapewe kwa ukamilifu wake bila ya upungufu. Na hapo wataujua kwa ujuzi wa yakini Ungu wa Mwenyezi Mungu na hukumu za Sharia yake, na ukweli wa ahadi yake na kitisho chake. Kwani yote hayo yatakuwa wazi hayana kificho.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Katika siku hiyo, Allah Mtukufu Atawalipa malipo yao kamili juu ya matendo yao kwa usawa, na watajua kwenye mkusanyiko huo mkubwa wa kisimamo kwamba Allah Mtukufu Ndiye Ukweli ulio wazi, Ambaye Yeye ni kweli, ahadi yake ni ya kweli, makemeo yake ni kweli, na kila kitu kitokacho kwake ni kweli, Ambaye hamdhulumu yoyote chochote hata kama ni kadiri ya uzani wa mduduchungu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net