An-Noor 24:22
النوروَلَا يَأْتَلِ أُو۟لُوا۟ ٱلْفَضْلِ مِنكُمْ وَٱلسَّعَةِ أَن يُؤْتُوٓا۟ أُو۟لِى ٱلْقُرْبَىٰ وَٱلْمَسَـٰكِينَ وَٱلْمُهَـٰجِرِينَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ۖ وَلْيَعْفُوا۟ وَلْيَصْفَحُوٓا۟ ۗ أَلَا تُحِبُّونَ أَن يَغْفِرَ ٱللَّهُ لَكُمْ ۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Na wale katika nyinyi wenye fadhila na wasaa wasiape kutowapa jamaa zao, na masikini na waliohama kwa Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wasamehe, na waachilie mbali. Je, nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu awasamehe? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wale katika nyinyi wenye fadhila na wasaa wasiape kutowapa jamaa zao na masikini na walio hama kwa Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wasamehe, na waachilie mbali. Je! Nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu akusameheni? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. [22]
[22] Wala wasiape wema wenu wenye nafasi kuwa watazuia kuwafanyia hisani jamaa zao na masikini na walio hama makwao katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wengineo kwa sababu za kibinafsi, kama vile kuwa wamewatendea uovu fulani. Lakini inatakikana wawasamehe na wayaachilie mbali makosa yao. Na ikiwa mnapenda Mwenyezi Mungu akusameheni maovu yenu basi wafanyieni wanao kufanyieni mabaya mfano wa anavyo kufanyieni nyinyi Mola wenu Mlezi. Na fuateni mwendo wake kwani Yeye ni Mkunjufu wa kusamehe na kurehemu. Aya hii imeteremka pale Abu Bakar r.a. alipo apa kumkatia msaada jamaa yake Mist'ah bin Uthaathah hapo alipo ingia Mist'ah katika uzushi alio zuliwa bibi Aisha r.a.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wala wasiape watu wema katika Dini na wakunjufu wa mali, kuacha kuwaunga watu wao wa karibu wasiokuwa na kitu, na wahitaji, na wageni waliohama makwao, na kuwanyima matumizi kwa sababu kuna kosa walilifanya. Basi na wayasamehe maovu yao wala wasiwatese. Kwani nyinyi hampendi Allah Mtukufu Awasamehe? Basi wasameheni. Allah Mtukufu ni Mwenye kuwasamehe waja Wake, ni Mwenye huruma kwao. Katika haya pana mahimizo juu ya kusamehe na kusahau kabisa, hata kama mtu atatendewa uovu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net