An-Noor 24:21
النوريَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّبِعُوا۟ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيْطَـٰنِ ۚ وَمَن يَتَّبِعْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيْطَـٰنِ فَإِنَّهُۥ يَأْمُرُ بِٱلْفَحْشَآءِ وَٱلْمُنكَرِ ۚ وَلَوْلَا فَضْلُ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُۥ مَا زَكَىٰ مِنكُم مِّنْ أَحَدٍ أَبَدًا وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ يُزَكِّى مَن يَشَآءُ ۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
Enyi mlioamini, msizifuate nyayo za Shetani. Na atakayefuata nyayo za Shetani basi yeye huamrisha machafu na maovu. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake juu yenu, asingelitakasika miongoni mwenu kabisa hata mmoja. Lakini Mwenyezi Mungu humtakasa amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Msizifuate nyayo za Shet'ani. Na atakaye fuata nyayo za Shet'ani basi yeye huamrisha machafu na maovu. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake juu yenu, asingeli takasika miongoni mwenu kabisa hata mmoja. Lakini Mwenyezi Mungu humtakasa amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. [21]
[21] Enyi mlio amini! Hifadhini nafsi zenu kwa Imani. Wala msimfuate Shetani anaye kuvutieni kwenda tangaza uchafu na maasi baina yenu. Na mwenye kumfuata Shetani basi huyo amekwisha a'si, kwani Shetani anaamrisha madhambi makubwa makubwa na maasi mabaya. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake kwenu kwa kubainisha hukumu na kukubali toba ya wenye kuasi asinget'ahirika hata mmoja wenu na uchafu wa maasi. Lakini Mwenyezi Mungu anamsafisha mwenye kumuelekea Yeye kwa kumwezesha kuwa mbali na maasi, au kwa kumsamehe kwa kutubu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia kila kauli, Mwenye kujua kila kitu, na atakulipeni kwayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazitekeleza sheria Zake, msifuate njia za Shetani. Na yoyote anayefuata njia za Shetani, basi (huyo Shetani) anamuamrisha vitendo viovu na vichafu. Na lau si wema wa Allah Mtukufu kwa Waumini na rehema zake kwao, asingetakasika yoyote katika wao na uchafu wa madhambi yake. Lakini Allah Mtukufu, kwa wema wake, Anamtakasa Anayemtaka. Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuyasikia maneno yenu, ni Mjuzi wa nia zenu na matendo yenu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net