An-Noor 24:20
النوروَلَوْلَا فَضْلُ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُۥ وَأَنَّ ٱللَّهَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ
Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake, na kuwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake, na kuwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole, Mwenye kurehemu. [20]
[20] Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake kwenu, na kuwa Yeye ni Mwingi wa upole, Mkunjufu wa rehema, asingeli kubainishieni hukumu, na angeli kuleteeni mateso kwa haraka hapa duniani kwa maasi yenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau kama si wema wa Allah Mtukufu juu ya wale waliohusika kwenye tukio la uzushi na rehema zake kwao na kwamba Allah Mtukufu Anawahurumia waja Wake Waumini huruma kunjufu katika yale wanaokuwa na pupu nayo (ya ulimwengu) na yale wanayoyasubiri (ya Akhera), asingefunua wazi hukumu hizi na mawaidha na angefanya haraka kumuadhibu yule aendaye kinyume na amri Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net