Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 19

An-Noor 24:19

النور

إِنَّ ٱلَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ ٱلْفَـٰحِشَةُ فِى ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ ۚ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

Maana

Kwa hakika wale wanaopenda uenee uchafu kwa walioamini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika wale wanao penda uenee uchafu kwa walio amini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui. [19]

[19] Hakika hao wanao penda kutangaza machafu, wakayatangaza baina ya Waumini watapata adhabu yenye kutia uchungu duniani kwa mateso yaliyo kwisha pasishwa, na Akhera watatiwa Motoni ikiwa hawato tubu. Na Mwenyezi Mungu anazijua vyema hali zenu zote, za dhaahiri na zilizo fichikana. Na nyinyi hamjui anayo yajua Yeye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika,wale wanaopenda kuenea machafu kwa Waislamu, ya tuhuma za uzinifu au jambo lolote baya, watapata adhabu kali ulimwenguni, kwa kupigwa mboko, na mengineyo miongoni mwa mitihani ya kilimwengu, na watapata adhabu ya Motoni huko Akhera wakiwa hawakutubia. Na Allah Mtukufu, peke Yake, Ndiye Anayejua urongo wao na Ndiye Anayeyajua maslahi ya waja wake na mwisho wa mambo, na nyinyi hamyajui hayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net