An-Noor 24:18
النوروَيُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمُ ٱلْـَٔايَـٰتِ ۚ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ
Na Mwenyezi Mungu anawabainishia Aya mbalimbali. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mwenyezi Mungu anakubainisheni Aya. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima. [18]
[18] Na Mwenyezi Mungu anakuteremshieni Aya zenye kuonyesha hukumu kwa uwazi dhaahiri. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu wa Ujuzi, hapana asicho kijua katika vitendo vyenu. Naye ni Mwenye hikima kwa kila anacho kitungia sharia na kukiumba. Kwani kila sharia zake na uumbaji wake ni kwa mujibu wa hikima.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Anawafafanulia nyinyi aya zinazokusanya hukumu za kisheria na mawaidha. Na Allah Mtukufu Anayajua sana matendo yenu, ni Mwenye hekima katika sheria Zake na uendeshaji Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net