An-Noor 24:23
النورإِنَّ ٱلَّذِينَ يَرْمُونَ ٱلْمُحْصَنَـٰتِ ٱلْغَـٰفِلَـٰتِ ٱلْمُؤْمِنَـٰتِ لُعِنُوا۟ فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ
Hakika wanaowasingizia wanawake, wanaojiheshimu, walioghafilika, Waumini; wamelaaniwa duniani na Akhera, nao watapata adhabu kubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wanao wasingizia wanawake, wanao jihishimu, walio ghafilika, Waumini, wamelaaniwa duniani na Akhera, nao watapata adhabu kubwa. [23]
[23] Hakika hao wanao wasingizia wanawake wema walio safi, ambao hawadhaniwi hayo, bali wao kwa kumshughulikia Mwenyezi Mungu hata wameghafilika na hayo wanayo singiziwa, Mwenyezi Mungu atawatenga mbali na rehema yake katika dunia na Akhera, na watapata adhabu kubwa ikiwa hawatotubu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa kweli wale wanaowasingizia kitendo cha uzinifu wanawake wenye kujihifadhi, wasiofikiria machafu na walio Waumini ambao halijawapitia jambo hilo kwenye nyoyo zao, hao ni wenye kufukuzwa kwenye rehema za Allah Mtukufu, duniani na Akhera, na watapata adhabu kubwa kwenye moto wa Jahanamu. Kwenye aya hii kuna ushahidi juu ya ukafiri wa mwenye kumtukana au kumtuhumu mke yoyote kati ya wake za Mtume, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, kwa jambo ovu lolote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net