Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 15

An-Noor 24:15

النور

إِذْ تَلَقَّوْنَهُۥ بِأَلْسِنَتِكُمْ وَتَقُولُونَ بِأَفْوَاهِكُم مَّا لَيْسَ لَكُم بِهِۦ عِلْمٌ وَتَحْسَبُونَهُۥ هَيِّنًا وَهُوَ عِندَ ٱللَّهِ عَظِيمٌ

Maana

Mlipoyapokea kwa ndimi zenu na mkasema kwa vinywa vyenu msiyoyajua, na mlifikiri ni jambo dogo, kumbe mbele ya Mwenyezi Mungu ni kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mlipo yapokea kwa ndimi zenu na mkasema kwa vinywa vyenu msiyo yajua, na mlifikiri ni jambo dogo, kumbe mbele ya Mwenyezi Mungu ni kubwa. [15]

[15] Mmezichukua khabari hizo kwa ndimi zenu na mkazieneza kati yenu. Wala nyinyi hamkujua kuwa hizo ni khabari za kweli, na mkaona jambo hili ni dogo si la kuadhibiwa na Mwenyezi Mungu, au sana adhabu yake ni ndogo; na ilhali ni jambo kubwa kweli la kuadhibiwa adhabu kali na Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kipindi mlichokuwa mnaupokea uzushi na mnaueneza kwa midomo yenu, nao ni yale maneno ya urongo na ambayo hamna ujuzi nayo. Na mambo mawili haya yameharamishwa: kusema maneno ya urongo na kusema bila ya ujuzi. Na mnadhani kuwa hilo ni jambo dogo, nalo ni kubwa mbele ya Allah Mtukufu. Katika haya pana makemeo bayana juu ya kupuuza makatazo ya uenezaji ubatilifu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net