An-Noor 24:16
النوروَلَوْلَآ إِذْ سَمِعْتُمُوهُ قُلْتُم مَّا يَكُونُ لَنَآ أَن نَّتَكَلَّمَ بِهَـٰذَا سُبْحَـٰنَكَ هَـٰذَا بُهْتَـٰنٌ عَظِيمٌ
Na kwa nini mlipoyasikia msiseme: Haitufalii kuzungumza haya. Subhanak! (Umetakasika!) Huu ni uzushi mkubwa!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwa nini mlipo yasikia msiseme: Haitufalii kuzungumza haya. Subhanak Umetakasika! Huu ni uzushi mkubwa! [16]
[16] Yanayo faa ni kuwa baada ya kusikia maneno haya ya uwongo ni kuambizana msiyazungumze, kwa sababu si laiki yenu, na mustaajabie kuzuliwa uwongo muovu wa namna hii wa khatari.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mbona hamkusema mlipousikia uzushi huo, «Haifai kwetu kuusema urongo huu. Kutakasika ni kwako, ewe Mola, kuyasema hayo juu ya mke wa Mtume wako Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). Huu ni urongo uliobeba mzigo mkubwa wa madhambi».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net