Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 24 · Aya ya 14

An-Noor 24:14

النور

وَلَوْلَا فَضْلُ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُۥ فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ لَمَسَّكُمْ فِى مَآ أَفَضْتُمْ فِيهِ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Maana

Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake katika dunia na Akhera, bila ya shaka ingeliwapata adhabu kubwa kwa sababu ya yale mliyojiingiza.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake katika dunia na Akhera, bila ya shaka ingeli kupateni adhabu kubwa kwa sababu ya yale mliyo jiingiza. [14]

[14] Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hakukufanyieni fadhila kwa kubainisha hukumu, na hakukurehemuni duniani kwa kuacha kuleta adhabu kwa haraka, na Akhera kwa kukusameheni, angeli kuteremshieni adhabu kubwa kwa sababu ya kujiingiza kwenu katika uzushi huu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau kama si wema wa Allah Mtukufu kwenu na rehema Zake, kwa kuwa wema Wake umewakusanya nyinyi katika Dini yenu na Akhera yenu, Asifanye haraka kuwaadhibu na aikubali toba ya mwenye kutubia miongoni mwenu, basi ingewapata adhabu kali kwa sababu ya maneno ya uvumi mliyojihusisha nayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Noor

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net