Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 67

Al-Muminoon 23:67

المؤمنون

مُسْتَكْبِرِينَ بِهِۦ سَـٰمِرًا تَهْجُرُونَ

Maana

Na huku mkiitakabari na usiku mkiizungumzia (Qur-ani) kwa dharau.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na huku mkitakabari na usiku mkiizungumza (Qur'ani) kwa dharau. [67]

[67] Na nyinyi katika mapuuza yenu mlikuwa mnatakabari na mnafanyia maskhara, mkiutaja huu Wahyi kwa sifa mbaya mnapo kutana katika taanusi zenu za usiku.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mnalifanya hilo na huku mnawaonesha watu kiburi pasi na haki kwa sababu ya Nyumba ya Allah Mtukufu tukufu. Mnasema, ‘Sisi ni watu wa Nyumba hiyo, hatushindwi tukiwa hapo,’ na mnakesha mkiwa kando kando yake kwa maneno maovu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net