Al-Muminoon 23:68
المؤمنونأَفَلَمْ يَدَّبَّرُوا۟ ٱلْقَوْلَ أَمْ جَآءَهُم مَّا لَمْ يَأْتِ ءَابَآءَهُمُ ٱلْأَوَّلِينَ
Je, hawakuifikiri kauli, au yamewajia ambayo hayakuwafikia baba zao wa zamani?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je, hawakuifikiri kauli, au yamewajia yasiyo wafikia baba zao wa zamani? [68]
[68] Je! Hawa wenye kupuuza wamekuwa wajinga hata hawakuizingatia Qur'ani wakaijua kwamba hii hakika ni Haki? Au huu wito wa Muhammad kwao umekuwa ni namna mbali kuliko walio kuja nayo Mitume wengine kwa kaumu zilizo kwisha tangulia walio ambao baba zao waliwawahi?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani hawayafikirii yaliyomo ndani ya Qur’ani, wakapata kujua ukweli wake, au limewazuia wao kuamini kwa kuwa wamejiwa na Mtume na kitabu ambacho mfano wake hakikuwajia baba zao wa mwanzo, wakakikanusha kwa ajili hiyo na wakakipa mgongo?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net