Al-Muminoon 23:66
المؤمنونقَدْ كَانَتْ ءَايَـٰتِى تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فَكُنتُمْ عَلَىٰٓ أَعْقَـٰبِكُمْ تَنكِصُونَ
Hakika zilikuwa Aya zangu mkisomewa, nanyi mkirudi nyuma juu ya visigino vyenu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika zilikuwa Aya zangu mkisomewa, nanyi mkirudi nyuma juu ya visigino vyenu, [66]
[66] Hamna udhuru. Kwani Aya zangu zenye kuteremshwa kwa wahyi zilikuwa mkisomewa, nanyi mkizipuuza kwa mapuuza yenye kugeuza hali zenu, na wala hamkuzisadiki, wala hamkuzifuata kwa vitendo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Zilikuwa aya za Qur’ani zikisomwa kwenu, ili mpate kuziamini, mnazikimbia hamtaki kuzisikia na kuzikubali na kuzifanyia kazi, kama anavyofanya mwenye kurudi nyuma kwa kule kurudi kwake nyuma.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net