Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 46

Al-Muminoon 23:46

المؤمنون

إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَإِي۟هِۦ فَٱسْتَكْبَرُوا۟ وَكَانُوا۟ قَوْمًا عَالِينَ

Maana

Kumwendea Firauni na wakuu wake. Lakini wakatakabari, nao walikuwa kaumu majeuri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kumwendea Firauni na wakuu wake. Lakini walijivuna, nao walikuwa watu majeuri. [46]

[46] Tuliwatuma wawili hao kwa Firauni na kaumu yake. Wakakataa kuamini kwa ajili ya takaburi, na wao ni watu walio kuwa wakisifika kwa kiburi, na majivuno, na ujeuri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Tuliwapeleka Mûsã na Hãrûn kwa Fir‛awn, hakimu wa Misri, na viongozi wa watu wake ambao walifanya kiburi wakakataa kumuamini Mûsâ na ndugu yake. Na wao walikuwa ni watu wanaojiona bora kuliko watu wengine, na walikuwa wakiwanyanyasa kwa kuwadhulumu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net