Al-Muminoon 23:45
المؤمنونثُمَّ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ وَأَخَاهُ هَـٰرُونَ بِـَٔايَـٰتِنَا وَسُلْطَـٰنٍ مُّبِينٍ
Kisha tukamtuma Musa na kakaye, Harun, pamoja na ishara zetu na hoja zilizo wazi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kisha tukamtuma Musa na nduguye, Haaruni, pamoja na ishara zetu na hoja zilizo wazi. [45]
[45] Kisha tukamtuma Musa na nduguye, Haaruni, tukawapa dalili za kukata kuthibitisha ukweli wa ujumbe wao, na hoja wazi yenye kudhihirisha kuwa wao ni kweli wametumwa kutoka kwangu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kisha tukampeleka Mûsã na ndugu yake Hârûn kwa alama zetu tisa, nazo ni fimbo, mkono, nzige, chawa, vyura, damu, mafuriko, shida za maisha na upungufu wa matunda, zikiwa ushahidi uliyo wazi wenye kuzishinda nyoyo, zipate kulainika kwa alama hizo nyoyo za waumini, na isimame hoja juu ya washindani.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net