Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 44

Al-Muminoon 23:44

المؤمنون

ثُمَّ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا تَتْرَا ۖ كُلَّ مَا جَآءَ أُمَّةً رَّسُولُهَا كَذَّبُوهُ ۚ فَأَتْبَعْنَا بَعْضَهُم بَعْضًا وَجَعَلْنَـٰهُمْ أَحَادِيثَ ۚ فَبُعْدًا لِّقَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ

Maana

Kisha tukawatuma Mitume wetu, mmoja baada ya mmoja. Kila umma alipowafikia Mtume wao, walimkadhibisha. Tukawafuatanisha hawa baada ya hawa, na tukawafanya kuwa hadithi za kusimuliwa. Basi wakapotelea mbali kaumu wasioamini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukawatuma Mitume wetu, mmoja baada ya mmoja. Kila umma alipo wafikia Mtume wao walimkanusha. Tukawafuatanisha hawa baada ya hawa, na tukawafanya ni hadithi za kusimuliwa. Wakapotelea mbali watu wasio amini. [44]

[44] Kisha tukawatuma Mitume wetu wakifuatana, kila mmoja kwa kaumu yake. Kila akija Mtume kwa kaumu yake waliukadhibisha wito wake. Nasi tukawateketeza mfululizo, na tukazifanya khabari zao ni hadithi za watu kusimuliana na kuzistaajabia. Basi hao kaumu wasio isadiki Haki wala hawaifuati wametengeka mbali na rehema, na wamehiliki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukawapeleka Mitume wetu waende kwa ummah hao, wakifuatana: hawa baada ya wengine. Na kila Mtume akiwalingania watu wake, wanamkanusha. Basi tukawafuatisha, kundi baada ya kundi, kwa kuwaangamiza na kuwamaliza, na hakuna kilichosalia isipokuwa ni habari za kuangamia kwao.Na tukazifanya habari hizo ni maneno ya kuzungumzwa na watu waliokuja baada yao, wakizichukua kuwa ni mazingatio. Basi maangamivu na kuepushwa na kila kheri ni kwa watu wasiowaamini Mitume wala kuwatii.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net