Al-Muminoon 23:47
المؤمنونفَقَالُوٓا۟ أَنُؤْمِنُ لِبَشَرَيْنِ مِثْلِنَا وَقَوْمُهُمَا لَنَا عَـٰبِدُونَ
Wakasema, "Je, tuwaamini watu wawili hawa kama sisi, na ambao kaumu yao ni watumwa wetu?"
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Je, tuwaamini wanaadamu wawili hawa kama sisi, na ambao watu wao ni watumwa wetu? [47]
[47] Wakasema kwa mastaajabu na kukanya: Je, tuuamini wito wa watu wawili walio ni wanaadamu kama sisi, na tena watu wao hawa Wana wa Israili ni wenye kutunyenyekea sisi na kutut'ii kama ni watumwa?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wakasema, «Je, tuwaamini watu wawili kama sisi, na jamaa zao Wana wa Isrâĩl wako chini ya amri yetu, wanatutii na wanajidhalilisha kwetu.?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net