Al-Muminoon 23:33
المؤمنونوَقَالَ ٱلْمَلَأُ مِن قَوْمِهِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَكَذَّبُوا۟ بِلِقَآءِ ٱلْـَٔاخِرَةِ وَأَتْرَفْنَـٰهُمْ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا مَا هَـٰذَآ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يَأْكُلُ مِمَّا تَأْكُلُونَ مِنْهُ وَيَشْرَبُ مِمَّا تَشْرَبُونَ
Na wakubwa katika kaumu yake, wale waliokufuru na wakakadhibisha mkutano wa Akhera, na tukawastarehesha katika uhai wa dunia hii, walisema: Huyu si chochote isipokuwa ni mtu kama nyinyi. Anakula katika mnavyokula, na anakunywa katika mnavyokunywa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wakubwa katika watu wake walioukufuru, na wakakanusha mkutano wa Akhera, na tukawadekeza kwa starehe, katika maisha ya dunia, walisem: Huyu si chochote ila ni mwanadamu kama nyinyi, anakula mlacho, na anakunywa mnywacho. [33]
[33] Na wakubwa katika kaumu yake walio kufuru na kukadhibisha kukutana na Mwenyezi Mungu na mambo ya Akheria ya hisabu na malipo, na tukawapa sehemu kubwa ya starehe na neema, wakasema kwa kukanusha wito wake, na kuwazuia watu wasimfuate: Hapana khitilafu yo yote baina ya Huud na nyinyi. Anakula chakula hicho hicho mnacho kila nyinyi. Na anakunywa vinywaji hivyo hivyo mnavyo vinywa nyinyi. Mfano wa huyu hawezi kuwa Mtume, kwa sababu hana sifa msizo kuwa nazo nyinyi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wakasema viongozi waliomkufuru Allah Mtukufu miongoni mwa watu wake na waliokataa kuwa kuna maisha ya Akhera na zikawafanya wakiuke mipaka zile neema walizoneemeshwa ulimwenguni za maisha ya anasa za kupindukia, Huyu anayewaita mumpwekeshe Allah Mtukufu, Aliyetukuka, si lolote isipokuwa ni mwanadamu kama nyinyi, anakula chakula cha aina mnachokula nyinyi, na anakunywa aina ya kinywaji mnachokunywa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net