Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 34

Al-Muminoon 23:34

المؤمنون

وَلَئِنْ أَطَعْتُم بَشَرًا مِّثْلَكُمْ إِنَّكُمْ إِذًا لَّخَـٰسِرُونَ

Maana

Kwa hivyo, nyinyi mkimtii mtu kama nyinyi, basi hakika mtakuwa hasarani.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na nyinyi mkimt'ii mtu kama nyinyi basi hakika mtakuwa khasarani. [34]

[34] Na wakawahadharisha kwa nguvu na mkazo, wakiwaambia: Mkimt'ii mtu aliye kama nyinyi kwa utu wake, basi nyinyi hakika mtakuwa mmekhasiri kwa kuwa hamtapata manufaa yo yote mkimfuata.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau mtamfuata binadamu kama nyinyi, basi nyinyi mtakuwa wakati huo ni wenye kupata hasara kwa kuwaacha waungu wenu na kumfuata yeye.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net