Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 32

Al-Muminoon 23:32

المؤمنون

فَأَرْسَلْنَا فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْهُمْ أَنِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُۥٓ ۖ أَفَلَا تَتَّقُونَ

Maana

Kisha tukawatumia Mtume miongoni mwao, kuwaambia: Muabuduni Mwenyezi Mungu! Hamna mungu yeyote asiyekuwa Yeye. Je, hamumchi?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Tukawapelekea Mtume miongoni mwao, kuwaambia: Muabuduni Mwenyezi Mungu! Hamna mungu asiye kuwa Yeye. Jee, hamwogopi? [32]

[32] Tukawapelekea Huud. Naye ni katika wao. Tukawaambia kwa ulimi wake: Muabuduni Mwenyezi Mungu peke yake. Kwani nyinyi hamna Mungu anaye stahiki kuabudiwa asiye kuwa Yeye. Ni Yeye peke yake anaye faa mumwogope. Basi, jee mmeikhofu adhabu yake mkimuasi?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Tukampeleka kwao Mtume miongoni mwao, naye ni Hûd, amani imshukie, akawaambia, «Muabuduni Allah Mtukufu, Peke Yake, hakuna muabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye. Je, hamuogopi mateso Yake mtakapomuabudu asiyekuwa Yeye?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net