Al-Muminoon 23:29
المؤمنونوَقُل رَّبِّ أَنزِلْنِى مُنزَلًا مُّبَارَكًا وَأَنتَ خَيْرُ ٱلْمُنزِلِينَ
Na sema: Mola wangu Mlezi! Niteremshe mteremsho wenye baraka, na Wewe ndiye Mbora wa wateremshaji."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na sema: Mola wangu Mlezi! Niteremshe mteremsho wenye baraka, na Wewe ni Mbora wa wateremshaji. [29]
[29] Na useme: Ewe Mola Mlezi! Nijaalie nishuke mashukio yenye baraka, pahala pazuri pa kukaa wakati wa kuteremka nchi kavu. Na unitunukie amani hapo. Kwani ni Wewe tu peke yako unaye weza kututeremsha pahala pa kheri na amani na salama.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na useme, «Mola wangu! nifanyie wepesi uteremkaji uliobarikiwa wenye amani, na wewe ndiye bora wa wenye kuteremsha.» Katika hili pana mafunzo kutoka kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka na kuwa juu, kwa waja Wake wasome dua hii wateremkapo mahali.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net