Al-Muminoon 23:28
المؤمنونفَإِذَا ٱسْتَوَيْتَ أَنتَ وَمَن مَّعَكَ عَلَى ٱلْفُلْكِ فَقُلِ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ٱلَّذِى نَجَّىٰنَا مِنَ ٱلْقَوْمِ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Basi utakapotulia sawasawa wewe na wale walio pamoja nawe humo merikebuni, sema: Alhamdulillahi (Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu), aliyetuokoa kutoka kwa kaumu madhalimu!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi utakapo tulia wewe na walio pamoja nawe humo marikebuni, sema: Alhamdulillahi Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, aliye tuokoa na watu madhaalimu! [28]
[28] Na ukisha panda na ukatua wewe na walio pamoja nawe katika jahazi hiyo basi sema kwa kumshukuru Mola wako Mlezi: Alhamdulillahi! Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye ndiye aliye tuokoa na shari ya watu makafiri walio asi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi ukiwa juu ya jahazi na ukatulia humo wewe na walio pamoja na wewe, mkiwa mmesalimika na kuzama, sema, ‘Shukrani zote ni za Allah Mtukufu Aliyetuokoa na watu makafiri.’
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net