Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 30

Al-Muminoon 23:30

المؤمنون

إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ وَإِن كُنَّا لَمُبْتَلِينَ

Maana

Hakika katika hayo zipo ishara. Na kwa yakini Sisi ni wenye kuwajaribu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika katika hayo yapo mazingatio. Na kwa yakini Sisi ni wenye kuwafanyia mtihani. [30]

[30] Hakika katika kisa hichi yapo mazingatio na mawaidha mengi. Na hakika Sisi tunawajaribu (tunawapa mitihani) waja wetu kwa kheri na shari. Na ndani ya nafsi zao wana utayarisho wa yote hayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika, katika kuwaokoa Waumini na kuwaangamiza makafiri, pana dalili za wazi zakuonesha ukweli wa Mitume wa Allah Mtukufu katika yale waliokuja nayo kutoka kwa Allah Mtukufu, na sisi ni wenye kuwapa mtihani watu kwa kuwapelekea Mitume kwao kabla mateso hayajawashukia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net