Al-Muminoon 23:26
المؤمنونقَالَ رَبِّ ٱنصُرْنِى بِمَا كَذَّبُونِ
Akasema (Nuhu), "Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa kuwa wamenikanusha."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema (Nuhu): Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa kuwa wamenikanusha. [26]
[26] Nuhu akamwomba Mola wake Mlezi baada ya kukata tamaa kuamini kwao, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ninusuru nao, na watie adabu kwa sababu ya kuukadhibisha kwao wito wangu!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Nûḥ akasema, «Mola wangu! Niokoe na watu wangu kwa sababu ya kunikanusha mimi kwa yale niliyowafikishia ya ujumbe wako».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net