Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 25

Al-Muminoon 23:25

المؤمنون

إِنْ هُوَ إِلَّا رَجُلٌۢ بِهِۦ جِنَّةٌ فَتَرَبَّصُوا۟ بِهِۦ حَتَّىٰ حِينٍ

Maana

Huyu si lolote isipokuwa ni mwanamume mwenye wazimu. Basi mngojeeni tu kwa muda."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Huyu si lolote ila ni mtu mwenye wazimu. Basi mngojeeni tu kwa muda. [25]

[25] Huyu si chochote ila ni mtu mwenye wazimu. Na kwa hivyo wakasema: Ngojeni, na mstahamilieni mpaka ukashifike wazimu wake, au kufike kuangamia kwake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na huyu Nûḥ hakuwa isipokuwa ni mwanamume aliyeshikwa na wazimu, basi ngojeeni mpaka atakapopata fahamu auache ulinganizi wake au afe mpumzike na yeye.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net