Al-Muminoon 23:24
المؤمنونفَقَالَ ٱلْمَلَؤُا۟ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِن قَوْمِهِۦ مَا هَـٰذَآ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُرِيدُ أَن يَتَفَضَّلَ عَلَيْكُمْ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ لَأَنزَلَ مَلَـٰٓئِكَةً مَّا سَمِعْنَا بِهَـٰذَا فِىٓ ءَابَآئِنَا ٱلْأَوَّلِينَ
Wakasema wale wakuu waliokufuru katika kaumu yake, "Huyu si chochote isipokuwa ni mtu tu kama nyinyi. Anataka kujipa ubora juu yenu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angetaka, basi kwa yakini angeliteremsha Malaika. Hatukusikia haya kwa baba zetu wa mwanzoni.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Walisema wale wakuu walio kufuru katika watu wake: Huyu si chochote ila ni mtu tu kama nyinyi. Anataka kujipa ubora juu yenu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu amependa basi yakini angeli teremsha Malaika. Hatukusikia haya kwa baba zetu wa zamani. [24]
[24] Wakubwa wa kaumu yake walio kufuru wakiukanya wito wake na wakizuia watu wasimfuate, walisema: Hapana khitilafu yoyote baina ya Nuhu na nyinyi. Kwani yeye ni mtu kama nyinyi, lakini anataka kujipa ubora juu yenu kwa huu wito wake. Na lau kuwa wapo Mitume wanao toka kwa Mwenyezi Mungu kama anavyo dai yeye, basi ange waletea Malaika. Sisi hatukupata kusikia wito huu katika taarikhi za baba zetu walio tangulia, wala kutumwa binaadamu kuwa ni Mtume.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi wale waheshimiwa wa watu wake walimkanusha na wakasema kuwaambia watu wa kawaida wao, Yeye ni mwanadamu kama nyinyi, hana ubora wowote wa kutafautiana na nyinyi, na hataki kwa maneno yake isipokuwa uongozi na utukufu juu yenu, na lau Allah Mtukufu angetaka kutuletea mtume, angemtuma Malaika kwetu, hatujasikia mfano wa hili kwa watu waliotutangulia miongoni mwa mababa na mababu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net