Al-Muminoon 23:116
المؤمنونفَتَعَـٰلَى ٱللَّهُ ٱلْمَلِكُ ٱلْحَقُّ ۖ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ ٱلْعَرْشِ ٱلْكَرِيمِ
Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki. Hakuna mungu yeyote isipokuwa Yeye, Mola Mlezi wa Kiti cha Enzi Kitukufu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki, hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A'rshi Tukufu. [116]
[116] Utukufu ni wa Mwenyezi Mungu peke yake. Na Yeye ndiye Mwenye kumiliki ufalme wote. Hapana Mwenye kuabudiwa kwa Haki isipo kuwa Yeye. Na Yeye ndiye Mwenye A'rshi Tukufu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ametukuka Allah Mtukufu Aliye Mfalme, Anayepelekesha kila kitu, Ambaye Yeye ni Kweli, ahadi Yake ni kweli, na onyo Lake ni kweli, na kila kitu kutoka Kwake ni kweli. Ametakasika na kuwa ataumba kitu kwa upuuzi au pasi na maarifa. Hapana mola isipokuwa Yeye, Mola wa ‘Arsh tukufu ambayo ndicho kiumbe kikubwa kuliko vyote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net