Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 117

Al-Muminoon 23:117

المؤمنون

وَمَن يَدْعُ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ لَا بُرْهَـٰنَ لَهُۥ بِهِۦ فَإِنَّمَا حِسَابُهُۥ عِندَ رَبِّهِۦٓ ۚ إِنَّهُۥ لَا يُفْلِحُ ٱلْكَـٰفِرُونَ

Maana

Na anayemuomba - pamoja na Mwenyezi Mungu - mungu mwenginewe, hana ushahidi wa hili; basi bila ya shaka hisabu yake iko kwa Mola wake Mlezi. Kwa hakika makafiri hawafanikiwi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na anaye muomba - pamoja na Mwenyezi Mungu - mungu mwenginewe hana ushahidi wa hili; basi bila ya shaka hisabu yake iko kwa Mola wake Mlezi. Kwa hakika makafiri hawafanikiwi. [117]

[117] Na mwenye kumuabudu mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu hana ushahidi wa kumfanya huyo astahiki kuabudiwa. Hakika Mwenyezi Mungu atampa adhabu kwa ushirikina wake bila ya shaka yoyote. Hakika makafiri hawaongokewi. Bali watao ongokewa ni Waumini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na yoyote atakayeabudu, pamoja na Allah Mtukufu Aliyepwekeka, mungu mwingine, asiyekuwa na hoja yoyote juu ya ustahiki wake kuabudiwa. Basi kwa kweli malipo yake juu ya kitendo chake hicho kiovu yako mbele ya Mola wake huko Akhera. Ukweli ni kwamba hakuna kufuzu wala kuokoka kwa makafiri Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net