Al-Muminoon 23:115
المؤمنونأَفَحَسِبْتُمْ أَنَّمَا خَلَقْنَـٰكُمْ عَبَثًا وَأَنَّكُمْ إِلَيْنَا لَا تُرْجَعُونَ
Je, mlidhani ya kwamba tuliwaumba bure, na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa?. [115]
[115] Je? Mlidhani kuwa tuliwaumbeni bila ya hikma, ndio mukafanya ufisadi katika ardhi, na mkadhani kuwa hamtafufuliwa mpate kulipwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je, mlidhania, enyi viumbe, ya kwamba sisi tuliwaumba nyinyi bure bure? hakuna maamrisho wala makatazo wala malipo mema wala mateso, na kwamba nyinyi hamtarudishw kwetu Akhera kwa Hesabu na Malipo?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net