Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 114

Al-Muminoon 23:114

المؤمنون

قَـٰلَ إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا ۖ لَّوْ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ

Maana

Atasema: Nyinyi hamkukaa huko duniani ila kidogo, laiti ingelikuwa mnajua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Atasema: Nyinyi hamkukaa huko duniani ila kidogo, laiti ingeli kuwa mnajua. [114]

[114] Basi Mwenyezi Mungu atawaambia: Hamkuishi duniani ila muda mchache tu. Na lau ingeli kuwa mnajua malipo ya ukafiri na uasi na kwamba starehe ya duniani ni chache mngeli amini na mkat'ii.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hapo atawaambia «hamkukaa isipokuwa kipindi kichache, na lau mngevumilia juu ya kumtii Allah Mtukufu mngefaulu kuipata Pepo, kama mngekua na ujuzi wa hilo.» Hivyo ni kwamba kipindi cha kukaa kwao duniani ni kichache sana kulingana na kipindi cha kukaa kwao Motoni milele.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net