Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 113

Al-Muminoon 23:113

المؤمنون

قَالُوا۟ لَبِثْنَا يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ فَسْـَٔلِ ٱلْعَآدِّينَ

Maana

Watasema: Tulikaa siku moja au sehemu ya siku. Basi waulize wanaoweka hisabu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watasema: Tulikaa siku moja au sehemu ya siku. Basi waulize wanao weka hisabu. [113]

[113] Watasema kwa kuyaona mafupi maisha yao kwa adhabu wanayo ikuta: Tuliishi muda wa siku moja au baadhi ya siku hivi. Basi waulize wanao weza kuhisabu, sisi tumeshughulishwa na hii adhabu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Watasema kwa kitisho cha Kisimamo na ukali wa adhabu, «Tulikuwa huko kwa siku moja au sehemu ya siku. Waulize washika hesabu wenye kuhesabu miezi na siku».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net