Al-Hajj 22:73
الحجيَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ضُرِبَ مَثَلٌ فَٱسْتَمِعُوا۟ لَهُۥٓ ۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ لَن يَخْلُقُوا۟ ذُبَابًا وَلَوِ ٱجْتَمَعُوا۟ لَهُۥ ۖ وَإِن يَسْلُبْهُمُ ٱلذُّبَابُ شَيْـًٔا لَّا يَسْتَنقِذُوهُ مِنْهُ ۚ ضَعُفَ ٱلطَّالِبُ وَٱلْمَطْلُوبُ
Enyi watu! Unapigwa mfano, basi usikilizeni. Hakika wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, hawawezi kuumba hata nzi ijapokuwa watajumuika kwa hilo. Na nzi akiwapokonya kitu, hawawezi kukiokoa kutoka kwake. Amedhoofika kweli huyo mwenye kutaka na mwenye kutakiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi watu! Unapigwa mfano, basi usikilizeni. Hakika wale mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, hawatoumba hata nzi ijapo kuwa watajumuika kwa hilo. Na nzi akiwapokonya kitu hawawezi kukipata kwake. Amedhoofika kweli huyo mwenye kutaka na mwenye kutakiwa. [73]
[73] Enyi watu! Sisi tunakufahamisheni ukweli wa ajabu, basi hebu usikilizeni na muuzingatie. Haya masanamu hayataweza kabisa kuumba chochote hata kikiwa kitu duni kabisa kama nzi; hata ikiwa yote yakisaidiana katika kuumba huko. Bali huyu makhluku duni kabisa akiwanyang'anya chochote katika hizo sadaka wanazo pewa masanamu hawawezi kumzuia au kumfukuza. Unyonge gani basi huo wa kushindwa na nzi kutoweza kurejesha alicho pokonya. Na nzi ni kitu dhaifu mno! Wote wawili ni wanyonge. Bali hayo masanamu ambayo kama mnavyo ona ni dhaifu zaidi, basi huwaje mwanaadamu mwenye akili akenda kuyaabudu na kutaka yamnafiishe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi watu! Kumepigwa mfano, usikilizeni na muuzingatie: Kwa hakika, masanamu na wanaodaiwa kufanana na Allah Mtukufu mnaowaabudu badala ya Allah Mtukufu, hawatoweza «hata wakijikusanya» kuumba nzi mmoja, basi itakuaje kuumba kikubwa zaidi? Wala hawawezi kukirudisha kitu alichokinyakua nzi kutoka kwao, Je kuna kuelemewa zaidi kuliko huko? Vyote viwili pamoja ni vinyonge: amedhoofika mtaka kurudisha kitu kilichochukuliwa na nzi kutoka kwake, naye ni yule muabudiwa badala ya Allah Mtukufu, na pia amedhoofika mtakwa, naye ni nzi. Basi vipi hawa masanamu na wanaofanywa kuwa wanafanana na Allah Mtukufu watafanywa ni waungu, ilhali wao wako kwenye udhaifu huu?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net