Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 72

Al-Hajj 22:72

الحج

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ ءَايَـٰتُنَا بَيِّنَـٰتٍ تَعْرِفُ فِى وُجُوهِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ٱلْمُنكَرَ ۖ يَكَادُونَ يَسْطُونَ بِٱلَّذِينَ يَتْلُونَ عَلَيْهِمْ ءَايَـٰتِنَا ۗ قُلْ أَفَأُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ مِّن ذَٰلِكُمُ ۗ ٱلنَّارُ وَعَدَهَا ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ۖ وَبِئْسَ ٱلْمَصِيرُ

Maana

Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, utaona chuki katika nyuso za waliokufuru. Hukaribia kuwavamia wale wanaowasomea hizo Aya zetu. Sema: Je, nikuambieni yaliyo mabaya zaidi kuliko haya? Ni Moto. Mwenyezi Mungu amewaahidi waliokufuru, na ni marudio mabaya hayo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanapo somewa Aya zetu zilizo wazi utaona chuki katika nyuso za walio kufuru. Hukaribia kuwavamia wale wanao wasomea hizo Aya zetu. Sema: Je! Nikwambieni yaliyo mabaya zaidi kuliko haya? Ni Moto. Mwenyezi Mungu amewaahidi walio kufuru, na ni marudio mabaya hayo. [72]

[72] Ewe Nabii! Hawa washirikina mtu akiwasomea Aya zetu zilizo wazi, na ambazo ndani yake mna ushahidi wa ukweli wa hayo unao waitia, na ubaya wa ibada zao, utaona katika nyuso zao ghadhabu na chuki inayo wajaa, hata inakaribia kuwapelekea kutaka kumuuwa huyo anaye wasomea. Ewe Nabii! Waambie kwa kuwazindua na kuwaonya: Je! Mtanisikiliza nikwambieni yaliyo kuwa mabaya zaidi kuliko hiyo chuki inayo kuunguzeni roho? Ni Moto ambao Mwenyezi Mungu amewaahidi walio kufuru kama nyinyi Siku ya Kiyama. Na hapana mwisho mbaya na makaazi maovu kuliko hayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na pindi zinaposomwa kwa washirikina aya za Qur’ani zilizo wazi, utauona uchukivu waziwazi kwenye nyuso zao, wanakaribia kuwapiga Waumini wanaowalingania kwa Allah Mtukufu Aliyetukuka na kuwasomea aya Zake. Basi waambie, ewe Mtume, «je, si niwape habari ya kitu chenye kuchukiza zaidi kwenu kuliko kuisikia haki na kuwaona walinganizi wake? Ni Moto ambao Allah Mtukufu Ameutayarisha kwa makafiri huko Akhera. Na mahali pabaya zaidi pa mtu kuishia ni hapo».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net